Shirika la Habari la Hawza - Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah aliwahi kusimulia kwamba: Wakati ambapo Hizbullah ilikuwa chini ya shinikizo kubwa kutoka kwa Israel na tulikuwa tunakabiliwa na matatizo mengi, tulikuwa tukimrejea Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi Mola amuhifadhi na tunamueleza kuhusiana na matatizo na hali inayo tukabili.
Naye alikuwa akituambia:
“Wakati mwingine katika kuendesha masuala ya nchi, kutatua baadhi ya mambo huwa ni jambo gumu sana kwangu, na njia yoyote haionekani. Hivyo nawaambia marafiki na jamaa wengine: Jiandaeni tuende Jamkaran.
Kwenye Msikiti Mtukufu wa Jamkaran, baada ya kujielekeza kwa dhati kwa Imamu wa zama (a.s), huhisi kwamba pale pale kuna mkono wa ghaibu ambao unanielekeza, na pale napata maamuzi, kisha natekeleza, na kwa njia hiyo tatizo huondoka.”
Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah alisema:
Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi Mola amuhifadhi kupitia kauli hiyo, alitutanabaisha sisi kwa Imamu wa zama (a.s).
Maoni yako